Jina la Yesu lipewe
sifa………..
Nakupenda sana msomaji
wa ukurasa huu wa NUKUU ZA MUNGU
Na wewe ni mtu wa pekee
sana kwangu, natambua uwepo wako katika kushirikiana nami kutangaza Neno la
Mungu.
Hivyo basi nahitaji
kushirikiana na wewe leo neno linahusu UPENDO!
Upendo huwezi kutokea
pasipo kuonesha ama kutambua thamani ya kile ukipendacho. Hivyo upendo ni hali
ya kuonesha kujali, kuthamini kitu ama MTU.
Upendo ni agizo
tulilopewa na Mungu, na kuthibisha hili Mungu alianza kutupenda sisi. “ Kwa
maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila
mtu mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele”. Yohana 3:16
Hii ni dhahili kabisa
kuwa UPENDO ni kitu chenye thamani
kinachoweza hata kugharimu uhai wa mtu. Lakini basi, ni nani awezae kuufuata
ule UPENDO aliotuonesha bwana Yesu
kwa kukubali kujitoa uhai wake kwa ajili ya maisha yetu? Jibu ni hakuna……….sio
mimi nasema bali “Hakuna aliye na upendo
mwingi kama huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.” Yohana
15:13
Hivyo basi Mungu kwa
kutambua madhaifu yetu na mapungufu yetu ametuagiza kupendana sisi kwa sisi,
kuchukuliana mizigo, kusaidiana matatizo kuona kila mmoja anathamani kwa
mwenzie, na hapo tutakuwa tunampenda Mungu. Kwani katika kitabu cha 1 Yohana
4:21 tunaagizwa “Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye mungu,
ampende na ndugu yake.” Hii inamaanisha kuwa mtu hawezi kumpenda Mungu kama
hajampenda ndugu yake kwanza.
Na humohumo kwenye
biblia inaongeza kwa kutuulizaa, Kama unaamchukia ndugu yako unaye muona,
Je, Mungu usiye muona utampendaje? Hivyo
upendo uanze kwetu sisi wenyewe.
Warumi 12:9,
inasisitiza kuwa upendo wetu usiwe wa kinafki, tupendane UPENDO wa kweli kwani pendo la kweli lina faida, linajenga
Amani, linaondoa Uongo, linaleta Baraka,
LINAONDOA DHAMBI.
Na katika UPENDO tutafika mbinguni, kwani
utatuweka karibu na Mungu na kutuweka mbali na dhambi.
Siku njema, na Mungu
akubariki kwa Upendo wake wa kweli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni