Jumatatu, 27 Aprili 2015

TUTAMBUE MAHALI SAHIHI PA KUELEZA SHIDA ZETU.



Habari za wakati huu,  ndugu msomaji katika ukurasa huu wa NUKUU ZA MUNGU.

Leo naanza kwa maswali mawili matatu hivi;

1.      Je unajua mahali sahihi pa kueleza shida zako?
2.      Je ni nani wakumueleza shida zako?
3.      Ipi ni njia sahihi ya kumaliza shida zako?

Wengi wamekuwa wakikosa majibu ya maswali haya, na kuanza kuhamisha imani zao kwa kupeleka shida zao kwa ndugu, majirani na wengine hata kudiriki kwenda kwa waganga wakiamini kupata suluhisho ya maswali yao.

Lakini leo nataka kuwapa jibu lililo sahihi ambapo tukianza kwa kuangalia katika kitabu cha Marko 11:24 “Kwa sababu hiyo nawaambia, yoyote myaombayo mkisali, amini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.”

Hivyo basi ndugu msomaji tunaelezwa kuwa kuwa NJIA iliyo sahihi yakueleza shida, mahitaji na matatizo yetu ni kwa njia ya MAOMBI, KUFANYA SALA kwa baba yetu yetu aliye MBINGUNI. Na si kama vile watu wanavyofikiri kueleza matatizo yao kwa ndugu ama kwa majirani na wengine kwenda kwa waganga.

Hiyo sio njia sahihi ndugu zangu, leo tunajifunza hili ili tupate kujua kuwa Mungu ndio msuluhishi wa matatizo yetu na sio mtu mwingine yeyote.

Mathayo 7:7 “Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni mtaona, bisheni nanyi mtafunguliwa.”  
  • ·         Wewe unaomba kwa nani?
  • ·         Unatafuta kwa nani?
  • ·         Unabisha kwa nani?
Ili kupata muafaka wa mahitaji yako?

Mungu wetu hashindwi na jambo Bwana, ebu nenda wazungu wanasema direct kwake mueleze mambo yako, muombe mahitaji yako, tafuta kwake kilicho chako, kapate haki yako.

Zungumza naye kwa upole, kuwa na ujasiri katika kumueleza mambo yako, naye atakujibu. Halleya!!!!!!!!!!!!!!!!!

Wengi wetu tunaharibu wenyewe, pasipo kujua. Tunahitaji Mungu atujibu mahitaji yetu huku mioyoni mwetu tumebeba mizigi isiyo mpendeza Mungu,  TUJIULIZE SISI KAMA WANADAMU NA KAMA MZAZI, MTOTO WAKO AMEKUKOSEA,  JE MTOTO  ATAPATAJE UJASIRI WAKUELEZA SHIDA ZAKE KWA MZAZI?

Na sisi kwa Mungu wetu ni watoto wake, tunapomkosea hukasirika sana. Hivyo tunakiwa kuomba msamaha ama kutubu dhambi zetu kabla ya kueleza shida zetu.

NDUGU MSOMAJI TUNACHOTAKIWA KUFAHAMU NI NAMNA YA KUENDENDA SAWASAWA MBELE ZA MUNGU, NAYE NI MWEMA KATIKA MAISHA YETU, ANASIKILIZA NA KUJIBU MAOMBI YETU. HIVYO TUJINYENYEKEESHE MBELE ZAKE NAYE ATATUJIBU.

BASI NIKUTAKIE WAKATI MWEMA WENYE BARAKA ZA MUNGU…………….
NATUKUTANE SIKU NYINGINE


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni