Habari za wakati huu ndugu msomaji wangu,
Na, Bwana
Yesu apewe sifa!
Leo tunaenda kujifunza juu ya MSAMAHA
Kwanza kabisa
tupate kufahamu MSAMAHA ni kitu
gani? “Neno “SAMEHE”
linamaanisha kusafisha nia au jambo nakulifanya kutokuwa na mawaa yoyote, ku
achilia, kufuatilia mbali deni”.
Tunapokosea mtu
uhuliza msamaha wake ili kurudisha uhusiano. Hapa tunaona kuwa msamaha huleta
upendo, huruma na neeema. Msamaha ni jambo la hiari mtu hutakiwi kulazimishwa
kutoa msamaha.
Neon la Mungu
linatuhitaji sisis wanadamu kuwasamehe wenzetu pale wanapotukosea, haijalishi
ni kosa la namna gani amekufanyia. Ila cha kushangaza wanadamu wa leo hatujui
kusamehe bali tunabaki kuhesabiana makosa ya watu waliokusea.
[ Mambo ya Walawi 19:18], “usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yakokama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana…….
Biblia inatuonyesha
vitu vinavyopelekea kukosekana kwa msamaha ni kinyongo na chuki juu ya mtu
mwingine. Lakini Mungun kupitia biblia bado anatu onya tusifanye visasi kwa
ndugu zetu, jirani zetu na hata watu wote wanaotuzunguka.
Kutoa msamaha kwa
walio tukosea ni Hazina kwetu siku ya mwisho tukikutana katika makao ya milele
mbinguni. Wengi hukata tamaa ya kusamehe wengine kwa kuwahesabia idadi ya
makosa walioyatenda, bali Mungu anatuelekeza kuwa Tusichoke kutoa misamaha kwa
waliotukosea hata kama wametukosea mara Elfu na Elfu. “ Kisha Petro akamwendea
akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikosea mara ngapi name nimsamehe? Hata mara
saba? Yesu akamwambia, sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini. [ Mathayo 18:21, 22].
Na tujiulize maswali kadhaa juu ya faida na hasara tutakazo zipata baada ya kutoa ama kutokutoa masaha kwa wengine? “ Kwa maaana mkiwasamehe watu makosa yao, na baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe ninyi watu makosa yao, wala baba yenu hatawasemehe ninyi makosa yenu.” [ Mathayo 6:14, 15]
Maisha yetu tunaanza kuyatengeneza tukiwa hapahapa Duniani, kwa maana mtun akipandacho ndicho atakachon kujan kukivuna. Hivyo ndugu zangu wakristo tujifunze kutoa misamaha kwa wengine ndipo na Baba yetu wa mbinguni atatusamehe na sisi makosa yetu.
Mungu hawezi kutusamehe, kama sisi hatuwezi kuwasamehe wengine. “ Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako” [ Isaya 43:25], na tuvae ule upendo wa Mungu kwetu, kwani Mungu akisamehe huwa hatkin kukumbuka yale tuliyo mkosea. Bali sisis binadamu tumezoea kutoa msamaha kwa kusema “ Nimekusamehe ila sitokusahau” , Mungu hapendi hivyo. Tukisamehe tuachilie na kusahau ndani ya mioyo yetu.
Msamaha utatusaidi kupata mafanikio ya Kiroho na Kimwili pia, kwani msamaha huleta Amani, Upendo, Baraka na Neema katika maisha yetu yote kiujumla.
Na Mungu akubariki,
Tukutane wakati mwingine wa Mungu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni