Jumatano, 29 Aprili 2015

MUNGU HUPENDA SIFA


Bwana Yesu apewe sifa,

Leo ni siku nyingine iliyo njema na ya kumpendeza Mungu.

Tumekuwa tukijifunza mengi sana yamuusuyo Mungu wetu, na leo tutaeenda kufahamu nini kuhusu SIFA kwa Mungu wetu.

SIFA ni kitendo cha kumtukuza, kumfanyia shangwe, kumuinua, kumshukuru kwa kutambua yale makuu aliyonayo na aliyokutendea wewe katika maisha yako yote.
Tukirudi katika maisha ya kawaida, ndani ya jamii zetu jamani watu tunapenda kusifiwa kwa yale makubwa na mazuri  tunayoyafanya. Au sivyo ndugu yangu? Eeeeh hata kwa yale madogo pia!!!!!!!

Basi tukirudi kwa Mungu wetu ni zaidi tena mno. MUNGU anapenda kutukuzwa na biblia inasisitiza kuwa “ katikati ya sifa Mungu ndio hushuka”. Lakini pia kuna njia nyingi ambazo watoto wa Mungu hupaswa kuzitumia katika kumsifu yeye. Nazo ni zipi?

“Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake. Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi; Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi; Msifuni kwa matoazi yaliayo; msifuni kwa matoazi yavumayo sana. Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya”. Zaburi 150
Katika kitabu hiki cha Zaburi tumeona mbinu mbalimbali, sababu nyingi na mahali ambapo tunatakiwa kumsifu Mungu.

Wengi watajiuliza maswali, Ni kwa nini tumpe Mungu sifa. Mungu akipewa sifa na akafurahi, hapo utupatia watu wake nguvu katika kushinda yale yanayotukabili katika maisha yetu. Kwa sababu Mungu akitutendea yaliyo mema inatupasa turudi kwake kwa ajili ya kumshukuru na hapo Mungu huona kuwa unatambua uweza wake na nguvu alizonazo hivyo basi atazidi kukuinua siku hadi siku katika maisha yako!

Hata wanadamu wakipewa sifa ndipo huzidisha juhudi katika kutenda yaliyo mazuri. Lakini kwa Bwana wetu Yesu kristo ni tofauti na wanadamu kwa sababu yeye hana ubaguzi hivyo humpatia kila mmoja kwa nafasi yake.

“Kwa kuwa furaha ya Bwana ni NGUVU zenu”. Nehemia 8:10b…………….. hivyo ndugu yangu tuzidi kumfurahisha Mungu wetu ili azidi kutuongezea nguvu katika maisha yetu.
Na kwa kumalizia tuone njia zingine za kumsifu Mungu, sio kwa kuimba tu, ama kucheza bali hata kwa
1.      Kwa matoleo [dhabihu za kushukuru ama sadaka ya shukrani]………………………Zaburi 50:23
2.      Kwa kumtumikia kikamilifu, mf; usafi kanisani, ujenzi wa kanisa yani shughuli zote za kikanisa kwa ujumla……………………….Zaburi 100:1,2
3.      Kwa njia ya maombi pia tunaweza kumsifu Mungu, na hapa wengi hukosea wakiamini kwenye Maombi ni wakati wa kueleza shida zao tu. La hasha tunatakiwa kufanya Maombi kwa ajili ya kumsifia Mungu wetu.

Mf. “ Mungu, wewe ni baba yetu, wewe ni Mungu uliyetukuka, ni Mungu wa kushinda wala hujui kushindwa na hujawahi kushindwa, umeoneka kuwa mwema katika maisha yangu siku hadi siku, na ndio maana sitoacha kukusifu katika yangu. Mungu wangu wewe ni mzuri, uzuri wako hako wa kuufananisha nao, maana wewe ni wa tofauti katika maisha ya wanadamu una upendo wa pekeee, haubagui ………………………………..” 
Huo ni mfano wa namna tunavyoweza kumsifia Mungu wetu kwa njia ya Maombi

Tunachotakiwa sasa nikumuahidi baba yetu wa Mbinguni kumsifu kweli katika maisha yetu yote ili nay eye aweze kutushindia. Haleluya watumishi wa Mungu……….
Basi tutasoma vitabu vifuatavyo kisha tutakuwa tumeweza kumuahidi Mungu kumrudishia sifa na utkufu wake. Zaburi 71:14,  71:8 na Zaburi 34:1

Na Mungu awabariki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni