Bwana Yesu apewe sifa,
Leo ni siku nyingine iliyo njema na ya kumpendeza
Mungu.
Tumekuwa tukijifunza mengi sana yamuusuyo Mungu
wetu, na leo tutaeenda kufahamu nini kuhusu SIFA kwa Mungu wetu.
SIFA
ni kitendo cha kumtukuza, kumfanyia shangwe, kumuinua, kumshukuru kwa kutambua
yale makuu aliyonayo na aliyokutendea wewe katika maisha yako yote.
Tukirudi katika maisha ya kawaida, ndani ya jamii
zetu jamani watu tunapenda kusifiwa kwa yale makubwa na mazuri tunayoyafanya. Au sivyo ndugu yangu? Eeeeh
hata kwa yale madogo pia!!!!!!!
Basi tukirudi kwa Mungu wetu ni zaidi tena mno. MUNGU anapenda kutukuzwa na biblia
inasisitiza kuwa “ katikati ya sifa Mungu ndio hushuka”. Lakini pia kuna njia
nyingi ambazo watoto wa Mungu hupaswa kuzitumia katika kumsifu yeye. Nazo ni
zipi?
“Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake;
Msifuni katika anga la uweza wake. Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa
kadiri ya wingi wa ukuu wake. Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa
kinanda na kinubi; Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;
Msifuni kwa matoazi yaliayo; msifuni kwa matoazi yavumayo sana. Kila mwenye
pumzi na amsifu Bwana. Haleluya”. Zaburi 150
Katika kitabu hiki cha Zaburi tumeona mbinu
mbalimbali, sababu nyingi na mahali ambapo tunatakiwa kumsifu Mungu.
Wengi watajiuliza maswali, Ni kwa nini tumpe Mungu
sifa. Mungu akipewa sifa na akafurahi, hapo utupatia watu wake nguvu katika
kushinda yale yanayotukabili katika maisha yetu. Kwa sababu Mungu akitutendea
yaliyo mema inatupasa turudi kwake kwa ajili ya kumshukuru na hapo Mungu huona
kuwa unatambua uweza wake na nguvu alizonazo hivyo basi atazidi kukuinua siku
hadi siku katika maisha yako!
Hata wanadamu wakipewa sifa ndipo huzidisha juhudi
katika kutenda yaliyo mazuri. Lakini kwa Bwana wetu Yesu kristo ni tofauti na
wanadamu kwa sababu yeye hana ubaguzi hivyo humpatia kila mmoja kwa nafasi
yake.
“Kwa kuwa furaha ya Bwana ni NGUVU zenu”. Nehemia 8:10b…………….. hivyo ndugu yangu tuzidi
kumfurahisha Mungu wetu ili azidi kutuongezea nguvu katika maisha yetu.
Na kwa kumalizia tuone njia zingine za kumsifu
Mungu, sio kwa kuimba tu, ama kucheza bali hata kwa
1. Kwa
matoleo [dhabihu za kushukuru ama sadaka ya shukrani]………………………Zaburi 50:23
2. Kwa
kumtumikia kikamilifu, mf; usafi kanisani, ujenzi wa kanisa yani shughuli zote
za kikanisa kwa ujumla……………………….Zaburi 100:1,2
3. Kwa
njia ya maombi pia tunaweza kumsifu Mungu, na hapa wengi hukosea wakiamini
kwenye Maombi ni wakati wa kueleza shida zao tu. La hasha tunatakiwa kufanya
Maombi kwa ajili ya kumsifia Mungu wetu.
Mf. “ Mungu, wewe ni baba yetu, wewe
ni Mungu uliyetukuka, ni Mungu wa kushinda wala hujui kushindwa na hujawahi
kushindwa, umeoneka kuwa mwema katika maisha yangu siku hadi siku, na ndio
maana sitoacha kukusifu katika yangu. Mungu wangu wewe ni mzuri, uzuri wako
hako wa kuufananisha nao, maana wewe ni wa tofauti katika maisha ya wanadamu
una upendo wa pekeee, haubagui ………………………………..”
Huo ni mfano wa namna
tunavyoweza kumsifia Mungu wetu kwa njia ya Maombi
Tunachotakiwa sasa
nikumuahidi baba yetu wa Mbinguni kumsifu kweli katika maisha yetu yote ili nay
eye aweze kutushindia. Haleluya watumishi wa Mungu……….
Basi tutasoma vitabu
vifuatavyo kisha tutakuwa tumeweza kumuahidi Mungu kumrudishia sifa na utkufu
wake. Zaburi 71:14, 71:8 na Zaburi 34:1
Na Mungu awabariki.